야고보서 1장 Swahili
일반서신 · James · Swahili · 27절
📝 이 장의 개요 흐름·핵심 구절·인물 더 보기 →
야고보서 1장은 야고보가 흩어진 열두 지파에게 보낸 인사로 시작한다. 시련 속의 인내, 믿음으로 지혜를 구하는 일, 욕심과 죄의 관계, 말씀을 듣기만 하지 않고 행하는 일, 참된 경건을 차례로 다룬다.
절 바로가기
1야고보서 · Swahili
1Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia ninyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salaam!
3kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu.
4Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
5Lakini kama mmoja wenu ametindikiwa hekima, basi, anapaswa kumwomba Mungu ambaye atampatia; kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na kwa ukarimu. 해설
6Lakini anapaswa kuomba kwa imani bila mashaka yoyote. Mtu aliye na mashaka ni kama mawimbi ya bahari ambayo husukumwa na kutupwatupwa na upepo. 해설
7Mtu wa namna hiyo, mwenye nia mbili na asiye na msimamo katika mwenendo wake wote,
8asidhani ya kwamba atapata chochote kile kutoka kwa Bwana.
9Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza,
10naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwa na Mungu. Maana tajiri atatoweka kama ua la porini.
11Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake.
12Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili atapewa tuzo la uzima ambalo Mungu aliwaahidia wale wanaompenda. 해설
13Kama mtu akijaribiwa, asiseme: "Ninajaribiwa na Mungu." Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote.
14Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya.
15Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.
16Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike!
17Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu.
18Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno lake la ukweli, ili tuwe namna ya matunda ya kwanza miongoni mwa viumbe vyake.
19Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika.
20Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki.
21Kwa hiyo, tupilieni mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu; jiwekeni chini ya Mungu na kupokea ule ujumbe uliopandwa mioyoni mwenu, ambao waweza kuziokoa nafsi zenu.
22Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo.
23Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo.
24Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo.
25Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.
26Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.
27Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Swahili
절을 누르면 복사·공유·형광펜·메모를 쓸 수 있습니다. 점선 낱말은 교회백과 문서로 이어집니다.
본문은 Swahili(스와힐리어) — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain) 형광펜·메모·읽은 표시는 판과 상관없이 같은 장에 함께 남습니다. 점선이 그어진 낱말은 교회백과에 문서가 있는 인물·지명·용어입니다(한 화면에 한 번씩만 표시). 형광펜·메모·읽은 표시는 이 브라우저에만 저장되며 내 표시에서 모아 볼 수 있습니다.
이 장의 구절 해설 문서 4
이 장을 언급한 문서
- 로마서 8장 28절 성경 구절
- 고린도전서 10장 13절 성경 구절
- 요한계시록 2장 10절 성경 구절
- 마태복음 6장 9-13절 성경 구절
- 마태복음 7장 7절 성경 구절
- 마가복음 11장 24절 성경 구절
- 야고보서 1장 2-4절 성경 구절
- 히브리서 2장 18절 성경 구절
- 야고보서 1장 12-14절 성경 구절
- 베드로후서 2장 9절 성경 구절
- 야고보서 4장 7절 성경 구절
- 말라기 3장 6절 성경 구절
- 디모데후서 4장 7-8절 성경 구절
- 요한계시록 2장 8-11절 성경 구절
- 베드로전서 1장 23절 성경 구절
- 히브리서 12장 6-11절 성경 구절
- 야고보서 1장 5-6절 성경 구절
- 누가복음 11장 2-4절 성경 구절
- 야고보서 4장 2-3절 성경 구절
- 야고보서 4장 11-12절 성경 구절
- 마태복음 7장 22-27절 성경 구절
- 마가복음 11장 22-25절 성경 구절
- 야고보서 2장 15-17절 성경 구절
- 마태복음 21장 21-22절 성경 구절
- 야고보서 1장 6-7절 성경 구절
- 창세기 4장 7절 성경 구절
- 야고보서 2장 21-24절 성경 구절
- 야고보서 2장 1-4절 성경 구절
- 에스라 7장 10절 성경 구절
- 심방 신앙생활
더 보기
글자 크기
바탕색과 글자색 (읽기 화면만)
글꼴
글자 두께
줄 간격
표시
읽어 주기 속도
읽어 주기